December 15, 2012
MANGULA KUREJEA NYUMBANI KWAKE NJOMBE KESHO, MAPOKEZI MAKUBWA AANDALIWA ZAIDI 1000 KUJIUNGA CCM
![]() |
| Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dr. Kikwete katikati akiteta jambo la makamu mwenyekiti bara BwPhilip Mangulla mjini Dodoma baada ya kuchaguliwa |
![]() |
| Magula siku alipotoka kijijini na kushiriki mkutano mkuu wa CCM Dodoma kama mjumbe wa kawaida |
![]() |
| Mangula alivyosasa hivi baada ya kuwa makamu mwenyekiti wa CCM bara |
Katibu
wa CCM mkoa wa Njombe Hosea Mpangike akionyesha ilani ya CCM wakati
akitoa ratiba ya ziara ya makamu mwenyekiti CCM Tanzania bara Philip
Mangula na kuelezea matumaini makubwa ya chama hicho kuendelea
kushinda katika chaguzi mbali mbali jana (picha na Francis Godwin)
Na Phesto Saidi, Njombe
WAKATI
wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa mpya wa Njombe
wameandaa mapokezi makubwa kesho kwa ajili ya kumpokea makamu mwenyekiti
wa CCM Tanzania bara Philip Mangulla anayerejea nyumbani toka alipopata
kushika nafasi hiyo kubwa ndani ya chama imeelezwa kuwa
nguvu ya chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mkoa Njombe
imeendelea kuteteleka zaidi .
Sehemu kubwa ya wakazi wa Njombe wameanza kuwa na imani kubwa ya safu mpya ya CCM na kupongeza kuchaguliwa kwa Mangulla na kupelekea jumla ya wanachama zaidi ya 1000 kutaka kukabidhiwa kadi za CCM na Mangulla pindi atakapopokelewa mkoani hapa .
Sehemu kubwa ya wakazi wa Njombe wameanza kuwa na imani kubwa ya safu mpya ya CCM na kupongeza kuchaguliwa kwa Mangulla na kupelekea jumla ya wanachama zaidi ya 1000 kutaka kukabidhiwa kadi za CCM na Mangulla pindi atakapopokelewa mkoani hapa .
Hata hivyo mbali ya kuteteleka huko kwa Chadema ambacho kilikuwa kitamba kuwa Njombe ni moja kati ya ngome zake kuu bado inaonyesha kubwa jinamizi la viongozi mbali mbali ndai ya Chadema kujiengua na chama hicho linaendelea kukiandama zaidi chama baada ya aliyekuwa mlezi wa Chama hicho mikoa ya kusini na aliyekuwa mgombea ubunge katika jimbo la Njombe Magharibi Thomas Nyimbo kujiweka kando na Chadema pamoja na makada wenzake zaidi ya watatu na baadhi ya viongozi kuanza kutamani kujiunga na CCM.
Katibu wa CCM mkoa wa Njombe Hosea Mpangike akizungumzia ujio wa Mangulla mkoani Njombe alisema kuwa ziara hiyo ni ya kwanza toka alipochaguliwa kuwa makamu mwenyekiti na kuwa mapokezi makubwa yameandaliwa ili kumpokea kiongozi huyo ambaye anarejea nyumbani na kufanya shughuli mbali mbali za chama.
Mpangike alisema kuwa wana CCM na wananchi wa mkoa wa Njombe wamekuwa na shauku kubwa ya kutaka kumwona kiongozi wao huyo hasa ukizingatia kuwa ni mara ya kwanza toka alipoondoka nyumbani kuelekea mjini Dodoma katika mkutano mkuu wa Taifa ambao ndio ulimchagua kushika nafasi hiyo.
Alisema Mangula atapokelewa mida ya saa 6 mchana katika mji wa Makambako ambapo mbali ya kuvalishwa skafu atapata nafasi ya kusalimiana na wananchi mbali mbali ambao wamepanga kujitokeza kumpokea pamoja na kupokea wanachama zaidi ya 500 katika mji huo wa Makambako .
Baada ya kuondoka Makambako mchana saa 8 atakuwa mjini Njombe katika ofisi ya CCM mkoa ambako atapata nafasi ya kufungua shina la wakereketwa ,kusaini kitabu cha wageni pamoja na kupokea taarifa ya chama kabla ya kusalimiana na wananchi na kupokea wanachama zaidi ya 500 pia ambao watakabidhiwa kadi za CCM na jioni saa 11 ataondoka Njombe kuelekea kijijini kwake Kinenulo kata ya Imalinyi kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu.
Hata hivyo Mpangike alimthibitishia mwandishi wa habari hizi kuwa hali ya upepo wa kisiasa katika mkoa wa Njombe imegeuka ghafla na matumaini ya Chadema kujigamba kuwa mkoa huo ni ngome yake yamepotea kwa nguvu zaidi baada ya ushahidi ulioonekana mara baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa CCM kushinda kwa kishindo dhidi ya Chadema iliyoambilia nafasi mbili kati ya nafasi 27 kwa uchaguzi wa vijiji na nafasi 3 kati ya nafasi 38 kwa uchanguzi wa vitongoji huku chama cha wananchi (CUF) wakiambulia nafasi moja pekee ya kitongoji.
Wakati huo huo mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amelazimika kusogeza mbele ziara yake jimboni Ludewa ili kushiriki mapokezi ya makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Bw Mangula.
Filikunjombe alisema kuwa aliona si vema kuanza ziara yake jimboni kabla ya kumpokea makamu mwenyekiti na kuwa ameamua kuungana na wana CCM wenzake katika mapokezi ya kiongozi huyo na baada ya kumpokea Mangula ndipo atakapoelekea jimboni kwake Ludewa kwa ajili ya kuanza ziara yake .
Hata hivyo Filikunjombe alisema kuwa safu ya viongozi wa sasa ndani ya CCM ni safu ambayo imekuwa ni tishio kwa vyama vya upinzani na kuwa ili CCM kuendelea kushinda zaidi katika chaguzi zijazo ni vema wana CCM kuendelea kuipa ushirikiano safu hiyo ambayo imeonyesha nia ya kweli ya kuleta mapinduzi ndani ya chama.



No comments:
Post a Comment