The best I town

www.phestothegreat.blogspot.com

Wednesday, September 10, 2014

HALI HATARISHI KWA WAKAZI WA MBEYA


HATARI TUPU TOCHI YA MBEYA YETU YAMULIKA BARABARA ZA CHUNYA: MALORI YATUMIKA KUBEBA MIZIGO NA ABIRIA ,USALAMA UPO?

Mbeya yetu iliwashuhudia Abiria hawa bila Kujali hatari wakiwa wanajipanga kupanda katika Gari la Mizigo huku kukiwa na usafiri wa usalama na wakutosha kabisa. Wakina mama wengine walikuwa na Watoto wao bila kujali afya zao kwa kuwa barabara hiyo ilikuwa na vumbi la kutosha.
Askari wa usalama barabarani akiwa kazini
Askari wa usalama barabarani akitumia mamlaka yake kulisimamisha Gari lililoshehena Mizigo na Abiria Juu
Hata hivyo uchunguzi umebaini Bajaji kubeba abiria ili kulisubiria Lori mbele kama inavyo onekana Pichani.
Cha Kushangaza zaidi hakuna abiria aliyeshushwa wala mizigo na kuamriwa kuendelea na Safari , Je hapa tuseme ni usalama wa barabarani au ni Hatari barabarani 
Kwa Furaha Abiria walioshushwa na Bajaji wakisubiri Lori kwa matumaini ili kuendelea na Safari yao.
Safari inaendelea bila wasi wasi kila Lori na Safari yake na kwa nafasi
Mizigo Imesheena na abiria wamesheena
Safari inaendelea bila wasi wasi ambapo Tulibaini kwa ukaribu kabisa Gari la kwanza la Mizigo likipita Ishara kuonesha kuwa liliruhusiwa pasipo na Pingamizi
Lori la pili nalo linapita nalo bila wasiwasi , Tazama hapo juu huyo abiria wa mbele alivyo jiegesha je Kuna tahadhari yotote hapa? Hapa pia tulibaini Askari wa usalama wa barabarani aliliruhusu bila kipingamizi
Na Hatimaye huku mbele tukashuhudia Mistubishi ambayo tuliiona ikiwa imesimamishwa na Askari wa usalama wa Barabarani nayo ikipita tena ikiwa na watu wengi ndani yake mpaka wengine hawajakaa  vizuri kama wanavyo onekana a


WAKATI Serikali na wadau mbali mbali nchini wakihaha kuepusha ajali zinazoendelea kuangamiza roho za watu, hali imekuwa tofauti kwa baadhi ya madereva na wamiliki wa vyombo vya usafiri.
 
Ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani umejitokeza mara nyingi Barabara za Mbeya-Chunya kupitia Kawetele na Mbeya-Mkwajuni Kupitia Mbalizi ambapo yamekuwa yakibeba abiria na mizigo licha ya kuwepo mabasi yaliyoruhusiwa Kisheria.

 Mbeya yetu imeshuhudia  magari matatu aina ya Fuso na Scania kubeba mizigo na kuning’iniza abiria juu jambo linalohatarisha usalama wa abiria na mali zao.
 
Magari hayo yalikutwa hivi karibuni  yakitokea jijini Mbeya na kuelekea Wilayani Chunya majira ya saa Tisa alasiri huku wasimamizi wa sheria za usalama barabarani na Sumatra wakiyaruhusu kuendelea na safari licha ya kuyaona yakifanya safari zake kila siku.
 
Mbeya yetu ilishuhudia magari hayo yenye namba za usajili T 168AZG aina ya Fuso, T 432 AAK aina ya Scania na T 646 BRQ aina ya Mitsubishi Fuso yakiwa yanapita barabarani eneo la Mwansekwa na kuyashuhudia yakipita Lwanjiro kwa ishara kuwa yaliruhusiwa kuendelea na safari.

Hata hivyo usalama wa abiria hao umekuwa mashakani licha ya Serikali kuimarisha barabara ya Mbeya-Chunya na kuwepo kwa magari ya abiria Lukuki yanayofanya safari zake kila siku na Sumatra kuamua kupunguza Gharama za usafiri. Ambapo awali walikuwa wakitozwa Tsh 10,000 kati ya Mbeya na Chunya na sasa nauli imefikia hadi Tsh 5,000. 
 
Hali hii Hatari huwa mbaya zaidi wakati wa minada inayofanyika maeneo mbalimbali katika Wilaya ya Chunya na Magari hiyo yamekuwa yakipita pembezoni mwa kituo cha Polisi cha Wilaya hiyo.


MBEYA INAULIZA JE WAHUSIKA MNALIONA HILI? NA TAMKO TUNANGOJA LITOLEWE HADI WAKATI WA MAAFA?

NDUGU MDAU KARIBU KUCHANGIA MAONI.

YALIYOJIRI KALENGA MKOANI IRINGA

MBUNGE MGIMWA ASEMA AMETUMIA ZAIDI YA TSH MILIONI 68 KWA MIENZI MITATU YA UBUNGE WAKE KUTEKELEZA AHADI ASILIMIA 90 ZA MBUNGE WA KALENGA ALIYEFARIKI DUNIA DR WILIAM MGIMWA

Mbunge wa  jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa  (kulia) akikabidhi ahadi ya bati 100 alizokuwa ameziahidi mbunge aliyepita marehemu Dr  Wiliam Mgimwa kwa  viongozi wa kijiji cha Mangalali kwa ajili ya ujenzi  wa vyumba vya madarasa  shule ya msingi Lukwambe hadi  sasa ni asilimia 90 ya ahadi binafsi za mbunge aliyefariki  zimetekelezwa jimbo la Kalenga na mbunge Mgimwa
mbunge wa Kalenga Godfrey Mgimwa akiongoza viongozi kutembelea  ujenzi wa zahanati kijiji cha Mangalali 
Diwani wa kata ya Ulanda kulia  akitoa ufafanuzi kwa mbunge wa  jimbo la Kalenga Bw Mgimwa  kuhusu maendeleo ya ujenzi wa zahanati kijiji cha Mangalali 
Katibu  wa mbunge Mgimwa kulia Bw Martine Simangwa  kulia akiteta jambo na mbunge Mgimwa 
Mwananchi  wa kijiji cha Mangalali akisalimia na mbunge wa jimbo la Kalenga  Bw Godfrey Mgimwa
Mbunge Mgimwa akidua sanjari na  wananchi wa kijiji cha Mangalali 
Mmoja kati ya  wananchi wa kijiji cha Mangalali akimpongeza mbunge Godfrey Mgimwa kwa  utendaji kazi mzuri 
Katibu wa Mgimwa akiwaonya  wana CCM wanaojipitisha  jimboni kwa  sasa 
Baadhi ya Wananchi wa  kijiji  cha Mangalali  wakiwa katika mkutano wa mbunge wao Bw Mgimwa



Mbunge wa  jimbo la Kalenga Bw Godfrey Mgimwa kulia akikabidhi mchango wake wa Tsh 250,000 kwa ajili ya kusaidia kazi ndogo ndogo  za ujenzi wa zanahati ya kijiji cha Mangalali 
 ........................................................................................................

MBUNGE   wa  jimbo  wa  jimbo la  Kalenga  Godfrey  Mgimwa  ajipongeza kutumia kiasi cha  zaidi ya Tsh milioni 68 kwa ajili ya  kufanikisha  utekelezaji wa ahadi  zilizotolewa na mbunge  aliyefariki Dr  Wiliam Mgimwa  kwa  asilimia 90 kwa  muda  wa  miezi mitatu pekee .

Akizungumza na  wananchi  wa  kijiji  cha Mangalali   baada ya  kukamilisha ahadi ya bati 100 kwa ajili ya ujenzi wa  vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Lukwambe , mbunge Mgimwa  alisema  kuwa alianza  kutekeleza  ahadi hizo hata kabla ya  kuapishwa   bungeni na  hadi sasa  bado asilimia 10 pekee ya utekelezaji wa ahadi zilizoachwa na mbunge  aliyefariki  dunia mwanzoni mwa mwaka  huu marehemu Dr Mgimwa ambae alikuwa ni babake mzazi.

" Ni jambo la kumshukuru  mwenyezi Mungu  kwani ahadi  zilizokuwa  zimetolewa na  mbunge  aliyefariki  dunia marehemu Dr  wiliam Mgimwa  zilikuwa ni asilimia 100 na hadi mnanichangua  kuwa  mbunge ahadi  hizo  zilikuwa  bado kutekelezwa na ndio  sababu ya mimi   katika kampeni kutoahidi  ahadi mpya  zaidi ya  kuzipokea  zile  zilizoachwa na baba ambazo  kimsingi nilizipokea .......ila kwa sasa ahadi  hizo nimetekeleza kwa asilimia 90  bado asilimia 10 pekee ambazo hadi mwakani  nitakuwa nimezimaliza kikubwa naomba mzidi kuniombea  uzima" alisema  mbunge Mgimwa.

Alisema  kuwa hakuweza  kuahidi ahadi mpya  wakati wa kampeni  hizo za uchaguzi mdogo  jimboni humo kutokana na kuwepo kwa ahadi nyingi ambazo  zilikuwa zimetolewa na mbunge  aliyepita na zilikuwa bado  kutekelezwa na muda  wa   utekelezaji  ulikuwa bado  hivyo aliamua  kuzichukua  zote kama  zilivyo na kuanza  kuzifanyia kazi moja baada  ya nyingine .

Mbunge Mgimwa alisema  kuwa ahadi  hizo  zinazotekelezwa  ni  zile ahadi  binafsi ambazo mbunge  aliyepita alikuwa amezitoa ila  zipo ahadi mbali mbali ambazo zimo katika ilani ya  CCM ambazo pia  zimeendelea  kutekelezwa  kwa  nguvu  kubwa .

Hata  hivyo  alisema kuwa ahadi ambazo  zimetekelezwa kwa asilimia 90 ambazo zilikuwa ni ahadi binafsi ni pamoja  na elimu ,afya na  uchangiaji wa  vikundi  vya Vicoba pamoja na uanzishwaji wa  vikundi  hivyo pia katika  sekta ya  michezo na huduma  nyingine  za kijamii kama  upelekaji wa umeme katika maeneo ya kata ya Mgama  na Magulilwa zoezi hilo  linaendelea ambayo   ahadi  hiyo ya umeme  ipo katika ilani ya CCM pamoja na zile za  huduma za maji vijijini ambazo baadhi ya maeneo mradi kata ya Maboga  na kata ya Lumuli wa maji  unatekelezwa .

Pia  alisema  kuwa bado  anautamani  ubunge wa  jimbo  hilo la Kalenga kwa mwaka 2015 -2020   hivyo kamwe hatawaangusha  wana Kalenga kwa  kipindi  hiki  cha miaka miwili alichopewa  hadi 2010.

" Ndugu  zangu hii nafasi ya  ubunge  mimi  nimeipata mwishoni ila sikutaka  kuwaangusha  nilitaka kuwaonyesha  utendaji  wangu na kamwe  sitakuwa mbali na ninyi  wananchi  wangu  nitakuwa  bega kwa  bega  kuhakikisha jimbo la Kalenga linapata maendeleo na linakuwa ni  jimbo la mfano katika maendeleo  kule  bungeni kutokana na umri  wangu  wabunge  wananiita bwana mdogo ila  kiutendaji kweli  ni bwana mkubwa kwani kati ya wabunge zaidi ya 300 bungeni  mimi ni mmoja kati ya  wabunge  tuliochanguliwa  kuingia katika kamati ya bunge ya bajeti ya  serikali " alisema mbunge Mgimwa .

Awali katibu  wa mbunge huyo  Martine Simangwa  aliwaonya  wana CCM ambao  wameendelea  kujipitisha katika  jimbo  hilo na kuwa kwa kufanya hivyo ni kutowatendea haki  wananchi wa  jimbo la Kalenga ambao kwa  sasa wameshikamana na  wapo tayari kuona  maendeleo na sio kampeni za  uchaguzi wa mwaka 2010.

"  wapo  baadhi ya  wana CCM bila haya  wameendelea  kujipitisha kwa wananchi na  kuponda utendaji huu mzuri wa mbunge Godfrey Mgimwa ....sasa  wananchi  nawaombeni  sana msidanganyike na  watu hao kwa sasa mbunge ni Godfrey Mgimwa wakija na kuwapa  pesa chukueni ila msikubali kugawanywa kwa misingi ya pesa kubalini  kuungana katika misingi ya kimaendeleo"

Kwa upande  wao  wananchi hao  walieleza  kufurahishwa na utendaji mzuri wa mbunge  wao Mgimwa na  kuwa kamwe hawatakubali kudanganyika na kuwa  wamejipanga  kumchukulia  fomu mwakani  ili kuwaongoza vipindi  vingine viwili zaidi baada ya  kuona utendaji  wake mzuri.

MWISHO 

Sunday, September 7, 2014

Friday, September 5, 2014

SALAM ZA RAMBI RAMBI KUTOKA TONE MULTIMEDIA GROUP KUTOKANA NA AJALI ILIYOTOKEA MUSOMA LEO.

 


PICHA KWA HISANI YA FATHER KIDEVU BLOG

Tone Multimedia Group ambao ni wamiliki wa Mtandao wa Blogs zamikoa TanzaniaTone Radio-TzThis Day Magazine na Matukio na wanavyuo, Tumepokea kwa masikitiko makubwa Taarifa za Ajali mbaya iliyotokea Musoma Ambayo ilihusisha  Basi la J4 Express  T677CYC lililokuwa linatoka Sirari kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi la Mwanza Coach T736AWJ  Tarehe 5.09.2014 Majila ya Mchana katika eneo la sabasaba Musoma wakati moja ya mabasi hayo likiovateki basi lengine  ambapo  watu zaidi ya 39 wamepoteza maisha huku wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa. Mpaka sasa Maiti 25 zimetambuliwa kati ya 39 na ndugu wa Marehemu.

Tunaungana na watanzania wote kuwapa pole ndugu waliopotelewa na Ndugu, Jamaa na Marafiki waliopoteza ndugu zao katika ajali hii, Pia tunawapa pole wale Majeruhi wote Tunawaombea kwa Mungu wapate kupona Haraka ili tuje kuweza kuungana nao katika Kujenga Taifa.

Imetolewa na uongozi
Tone Multimedia Group

Saturday, December 15, 2012


December 15, 2012

MANGULA KUREJEA NYUMBANI KWAKE NJOMBE KESHO, MAPOKEZI MAKUBWA AANDALIWA ZAIDI 1000 KUJIUNGA CCM

 Mwenyekiti  wa CCM Taifa  Rais Dr. Kikwete katikati  akiteta jambo la makamu mwenyekiti bara BwPhilip Mangulla mjini Dodoma baada ya kuchaguliwa
Magula siku  alipotoka  kijijini na kushiriki mkutano mkuu wa CCM Dodoma kama mjumbe wa kawaida

Mangula alivyosasa  hivi baada ya  kuwa makamu mwenyekiti wa CCM bara



Katibu  wa  CCM mkoa wa Njombe Hosea Mpangike akionyesha ilani ya CCM  wakati  akitoa ratiba ya  ziara ya makamu mwenyekiti  CCM Tanzania bara Philip Mangula na kuelezea matumaini makubwa ya chama hicho  kuendelea  kushinda katika chaguzi mbali mbali jana (picha na Francis Godwin)

Na  Phesto Saidi, Njombe
WAKATI wanachama  wa  chama cha mapinduzi (CCM)  mkoa  wa mpya  wa Njombe  wameandaa mapokezi makubwa  kesho  kwa ajili ya  kumpokea makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Philip Mangulla anayerejea  nyumbani toka alipopata kushika nafasi hiyo kubwa ndani ya chama imeelezwa  kuwa nguvu  ya chama cha  Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)  mkoa   Njombe imeendelea kuteteleka zaidi .

Sehemu kubwa ya wakazi  wa Njombe  wameanza kuwa na imani  kubwa ya  safu  mpya ya CCM na  kupongeza kuchaguliwa kwa  Mangulla na kupelekea jumla ya wanachama zaidi ya 1000 kutaka  kukabidhiwa kadi  za CCM  na   Mangulla  pindi atakapopokelewa mkoani hapa  .
Duru  za  kisiasa  katika mkoa  wa Njombe  zinadai  kuwa moja  kati ya dalili mbaya  kwa Chadema katika mkoa  wa Njombe ni  matokeo ya uchaguzi  wa serikali za mitaa ambao umefanyika  mara  baada ya wajumbe wa mkutano mkuu  wa CCM kumpitisha kwa  kishindo mwenyekiti  wa CCM Taifa  Rais Dkt Jakaya  Kikwete pamoja na makamu mwenyekiti  huyo Mangulla kwa upande wa bara  na  kupelekea  wanachama  wa  vyama  vyote kuungana  kuchagua viongozi kutoka CCM na Chadema  kujikuta  ikiambulia  vitongoji  3 katika ya 38 huku CUF ikiambulia kitongoji kimoja na  CCM ikivigalagaza vyama  vya upinzani kwa  kupata  vitongoji 34 na  mitaa 25 kati 27 kuchukuliwa na CCM na Chadema kupata  mitaa miwili  pekee.

Hata  hivyo mbali ya  kuteteleka  huko kwa Chadema ambacho kilikuwa  kitamba  kuwa  Njombe ni moja kati ya  ngome  zake kuu bado inaonyesha kubwa  jinamizi  la  viongozi  mbali mbali ndai ya  Chadema  kujiengua na chama  hicho linaendelea kukiandama  zaidi  chama baada ya aliyekuwa mlezi  wa Chama  hicho mikoa ya kusini na aliyekuwa  mgombea ubunge katika  jimbo la Njombe Magharibi Thomas Nyimbo kujiweka kando na Chadema pamoja na makada  wenzake zaidi ya  watatu  na baadhi ya viongozi kuanza kutamani kujiunga na CCM.

Katibu  wa CCM mkoa  wa Njombe Hosea Mpangike  akizungumzia  ujio  wa Mangulla mkoani Njombe  alisema  kuwa ziara  hiyo ni ya kwanza  toka  alipochaguliwa  kuwa makamu mwenyekiti  na kuwa mapokezi makubwa  yameandaliwa  ili  kumpokea  kiongozi huyo ambaye anarejea  nyumbani na  kufanya  shughuli mbali mbali  za chama.

Mpangike  alisema  kuwa  wana CCM na wananchi  wa mkoa  wa Njombe wamekuwa na shauku kubwa ya  kutaka  kumwona kiongozi  wao huyo hasa  ukizingatia  kuwa ni mara ya kwanza  toka alipoondoka nyumbani kuelekea  mjini Dodoma katika  mkutano mkuu  wa Taifa ambao  ndio  ulimchagua  kushika nafasi hiyo.

Alisema  Mangula atapokelewa mida ya saa 6 mchana  katika  mji  wa Makambako ambapo  mbali ya  kuvalishwa  skafu atapata  nafasi ya  kusalimiana na  wananchi mbali mbali ambao wamepanga  kujitokeza  kumpokea pamoja na  kupokea  wanachama  zaidi ya 500 katika mji  huo wa Makambako .

Baada ya kuondoka Makambako mchana  saa 8 atakuwa mjini Njombe katika ofisi ya CCM mkoa ambako atapata nafasi ya  kufungua shina la  wakereketwa ,kusaini  kitabu cha wageni  pamoja na  kupokea taarifa ya chama kabla ya  kusalimiana na wananchi na kupokea  wanachama zaidi ya 500 pia ambao  watakabidhiwa kadi  za  CCM na jioni saa 11 ataondoka Njombe kuelekea kijijini kwake Kinenulo kata ya Imalinyi kwa ajili ya mapumziko ya  sikukuu.

Hata  hivyo Mpangike alimthibitishia  mwandishi  wa habari hizi kuwa hali ya  upepo wa kisiasa katika mkoa  wa Njombe  imegeuka  ghafla na matumaini ya Chadema  kujigamba kuwa  mkoa huo ni ngome yake yamepotea kwa nguvu zaidi baada ya ushahidi  ulioonekana mara baada ya uchaguzi  wa serikali za mitaa kwa  CCM kushinda kwa  kishindo  dhidi ya Chadema  iliyoambilia nafasi  mbili kati ya nafasi 27 kwa uchaguzi  wa vijiji na nafasi  3 kati ya nafasi  38 kwa uchanguzi  wa vitongoji  huku chama cha  wananchi (CUF) wakiambulia nafasi moja  pekee ya kitongoji.

Wakati  huo  huo mbunge  wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amelazimika  kusogeza  mbele  ziara  yake jimboni Ludewa ili kushiriki mapokezi ya makamu mwenyekiti  wa CCM Tanzania  Bara Bw Mangula.

Filikunjombe alisema  kuwa aliona si vema  kuanza  ziara  yake  jimboni kabla ya kumpokea makamu  mwenyekiti  na kuwa ameamua  kuungana na wana CCM wenzake katika mapokezi ya kiongozi  huyo na baada ya  kumpokea Mangula ndipo atakapoelekea  jimboni kwake  Ludewa kwa ajili ya  kuanza  ziara  yake .

Hata  hivyo Filikunjombe  alisema  kuwa safu ya  viongozi  wa sasa ndani ya CCM ni safu ambayo  imekuwa ni tishio kwa  vyama vya upinzani na  kuwa ili CCM kuendelea  kushinda  zaidi katika chaguzi zijazo ni  vema  wana CCM kuendelea  kuipa ushirikiano safu  hiyo ambayo imeonyesha nia ya  kweli ya kuleta mapinduzi ndani ya chama.

Thursday, December 6, 2012

MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA MWANGOSI AKWAMA MAHABUSU TENA Huyu ndie mtuhumiwa wa mauwaji ya Daudi Mwangosi MTUHUMIWA wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel Ten Daud Mwangosi aliyetakiwa kufikishwa mahakamani kwa mara nyingine kutokana na sababu ya magari ya kubebea mahabusu kukosa mafuta. Mwandishi wa mtandao huu kutoka Iringa Gustav Chahe anaripoti kuwa ,Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia wengine waliokuwa na silaha mbalimbali huku wengine wakivaa kiraia waliweka ulinzi mkali kuhakikisha waandishi wa habari hawapati mwanya wa kupiga picha. Mwendesha mashtaka wa serikali Adolf Maganda aliambia mahakama mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Dyness Lyimo kuwa mtuhumiwa hakufikishwa mahakamani kutokana na magari ya kuwabeba mahabusu yamekosa mafuta. Hata hivyo Maganda alisema upelelezi haujakamilika na kesi imeahilishwa hadi 19 Desemba mwaka huu. Pasificus Cleophace Simon (23) alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kwa tuhuma ya kumuua kwa makusudi mwandishi huyo katika ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa uliofanyika Septemba 2 mwaka huu. Siku ya kwanza mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa gari la kifahari lenye namba za kiraia T 320 ARC linalosadikiwa kuwa ni la RCO huku kwa mara ya pili akifikishwa kwa miguu na kuondolewa mahakamani hapo kwa gari namba DFP 2175 pick up akiwa katika ulinzi mkali huku waandishi wa habari wakidhibitiwa na polisi na mmoja wao kunusurika kupigwa jambo lililozusha hisia tofauti miongoni mwa wananchi wengi mkoani hapa. Hii ni mara ya pili kwa mtuhumiwa huyo kutokufikishwa mahakamani kutokana na sababu ya magari kukosa mafuta japo kuwa kwa wakati huu hakuna tatizo la mafuta kama kipindi cha mwanzo. Mwangosi aliuawa kwa bomu Septemba 2 mwaka huu katika kijiji cha Nyololo yo alipokuwa akiwajibika kwa kazi za kihabari wakati wa ufunguzi wa matawi hayo. ……………………………… Mwisho …………………………

December 6, 2012

ALAZIMIKA KUUZA GARI ILI KUOKOA MAISHA YA MAMA MKWE ,JITOKEZENI KUNUNUA



Nimekutwa na matatizo na ninahitaji kapesa kidogo hivyo nalazimika kuuza kausafiri kangu (pichani) ili nimuuguze mama mkwe.

Kwa wadau wanaohitaji :

Bei sh TZS 4,5M

Mawasiliano :0713113048

Innocent Usangira
Email: usangira@gmail.com
P.O.Box 75854, Dar es Salaam-Tanzania
Cell: +255 754 711 959
+255 713 113 048
+255 684 384 838

MWANDISHI WA HABARI APIGWA RISASI NA JESHI LA POLISI




Shaban Matutu
Mwanahabari mwingine  mkoani Dar es Salaam apigwa  risasi na askari  polisi ambao  wanadaiwa  kuwa  walikuwa  wakimsaka mtuhumiwa  wa ujambazi  mwanamke na kuishia kumpiga mwanahabari  huyo mwanaume  Bw  Shaban Matutu wa gazeti la Tanzania  Daima.
Tukio  hilo limetokea jana majira  ya saa 2 usiku  jijini  Dar es Salaam ambapo askari  hao walipofika  nyumbani  kwa  mwanahabari  huyo na  kumgongea mlango na  wakati akifungua mlango ndipo

 Matutu amepigwa risasi na Polisi, ambao wanadaiwa walikuwa wanamtafuta mhalifu ambapo katika zoezi hilo, walienda na kugonga chumbani kwa Mwandishi huyo, kabla ya kutwanga kwa risasi.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, mara baada ya tukio hilo, mwandishi huyo amekimbizwa hospitali ya Mwananyamala ambako anaendelea kupatiwa huduma ya haraka na inaelezwa kuwa, amejeruhiwa lakini hali yake si mbaya sana
Habari zaidi zitakujieni

Taarifa za uhakika na ambazo zimethibitishwa­ zinaeleza kuwa jana usiku polisi mwenye silaha, aina ya bastola alimjeruhi begani kwa risasi, mwandishi wa habari wa Tanzania Daima, Shaaban Matutu.

Risasi bado imenasa kwenye bega lake hadi sasa Matutu alipigwa risasi nyumbani kwake Kunduchi, Dar es Salaam wakati askari walipovamia nyumba yake kwa madai kwamba kuna kibaka aliingia kujificha nyumbani hapo. Hivi sasa Matutu anatibiwa Mwananyamala hospitali, lakini amepewa rufaa kwenda Muhimbili.

Mwenyekiti  wa  jukwaa la wahariri Tanzania Bw Absalom Kibanda, ambaye amefanya jitihada za kumuhamishia Matutu Muhimbili, anasema hali ya Matutu siyo nzuri na kwamba wanajipanga kwenda Muhimbili kuona iwapo risasi hiyo itaondolewa mwilini.

Hata  hivyo  Kibanda ameeleza  kusikitishwa kwake ni  vitendo vya uvunjifu wa amani dhidi ya  wanahabari nchini Tanzania ambavyo  vimeendelea kufanywa na jeshi la  Polisi nchini na kutaka polisi  waliofanya  hivyo  kuchukuliwa hatua  kali.

Alisema wakati Taifa likiwa bado katika majonzi ya  mauwaji ya  kinyama ya Mwandishi wa Chanel Ten mkoa wa Iringa Daudi Mwangosi leo  tunashudia tena unyama mwingine dhidi ya  mwanahabari  huyo.

Hivyo  iwapo jeshi la  polisi litakosa majibu juu ya sababu ya  kumpiga risasi mwanahabari  huyo ambaye hata  hivyo hakuwa mlengwa katika msako wao  wa kumsaka mtuhumiwa wa ujambazi ambae ni mwanamke basi itafika  sehemu  wanahabari nchini  watalichukulia jeshi la polisi ni maeneo ya hatari kwao